Apu maalum ya Android ya Wikipedia iliyobuniwa kusaidia kupata, kufichua na kupeleleza maarifa iliyo Wikipedia. Suluhisha dau na rafiki yako kwa kutafuta haraka kwenye apu, ama zamia kwenye makala yaliyoangaziwa, picha, nakala iliyopendekezwa na mengine mengi kwa kutumia bibu ya upelelezi. Kwa zaidi ya makala milioni 39 katika takriban lugha 300, ensaiklopidia yako ya mtandaoni unayoipenda zaidi iko mikononi mwako.

Vipengele:

Uwezo wa kutafuta kwa sauti - Pata kwa urahisi unachokitafuta kwa upau maarufu wa utafutaji juu ya apu, ikiwa pamoja na utafutaji unaowezeshwa kwa kutamka kwenye kifaa chako.

Karibu -Pata maelezo zaidi kuhusu kile kilicho karibu nawe kwa kuchagua pointi kwenye ramani shirikishi ili kuona makala zinazohusiana na eneo lako la sasa na la karibu.

Jedwali la yaliyomo - telezesha kidole kushoto kwenye makala yoyote ili kuleta jedwali la yaliyomo, ambayo hukuruhusu kuruka hadi sehemu za makala kwa urahisi.

Orodha za kusoma - Panga makala unazovinjari katika orodha za kusoma, ambazo unaweza kufikia hata ukiwa nje ya mtandao. Unda orodha nyingi upendavyo, zipe majina na maelezo maalum, na uzijaze na makala kutoka kwa wiki yoyote ya lugha.

Ufafanuzi kutoka kwa Wiktionary - Gusa-na-ushikilie ili kuangazia neno, kisha uguse kitufe cha "Define" ili kuona ufafanuzi wa neno kutoka Wiktionary.

Wikipedia Zero - Fikia Wikipedia ya Android bila malipo ya data kwa waendeshaji wa simu wanaoshiriki. (kiungo kwa waendeshaji wanaoshiriki).

Tuma maoni yako kuhusu apu! Kwa menu,bonyeza "Settings", kisha" About the wikipedia app",kisha "Send app feedback".

Sera ya faragha: https://m.wikimediafoundation.org/wiki/Privacy_policy

Sera ya faragha ya watoa huduma wengine wa ripoti ya kuacha kufanya kazi:https://www.microsoft.com/en-us/privacystatement/OnlineServices/Default.aspx

Masharti za kutumika: https://m.wikimediafoundation.org/wiki/Terms_of_Use

Kuhusu Msingi wa Wikimedia

Msingi wa Wikimedia ni shirika lisilo la faida linalo fadhili Wikipedia na miradi mingine ya Wikimedia. Msingi huu ni wa hisani na hufadhiliwa hasa kwa michango. Kwa maelezo zaidi, zuru tovuti yetu:https://wikimediafoundation.org/wiki/Home.
