Soma taarifa yaliyohifadhiwa kwenye misimbo pau au ujenge misimbo ya QR ya kugawiza anwani, wawasiliani ama maandiko kati ya vifaa.

Upekuzi wa vitabu, bidhaa na wa wavuti unaelekezwa kwenye seva ya Google (kulingana na nchi asili iliyochaguliwa), kupitia kitufe cha kutafuta kinachotenegenezwa kwa mipangilio, kwa mfano duckduckgo.com/?q=%s ama wikibooks.org/w/index.php?search=%s.

Inawezesha aina zifuatazo za misimbo pau:

*UPC-A na UPC-E
*EAN-8 na EAN-13
* Kanuni 39;93;128
*ITF
*Codabar
*RSS-14(aina zote)
*Msimbo wa QR
*Matriki ya data
* Aztec('beta' kwa ubora)
*PDF 417('alfa' kwa ubora)

Angalia tovuti ili upate tafutajishida na maelezo ya ruhusa. Apu inakuruhusu ugawize wawasiliani, apu na vialamisho kwenye msimbo wa QR. Hii ndio maana ruhusa za wawasiliani zinahitajika. Angalia "Tembelea Tovuti ya Msanidi programu" ifuatayo ( https://github.com/zxing/zxing/wiki/Frequently-Asked-Questions ).

Kama chombo chako hakikagui, kwanza jaribu mbadala kwenye hitilafu za kifaa kwa mipangilio. Wezesha yote, kisha jaribu kuondolea uwezo moja kwa moja ili kujua ni gani inahitajika. Kama hii haisaidii, jaribu kufuta akiba ya kifaa na mipangilio kutoka kwa mipangilio ya Android.

Kama njia zote zimeshindikana na unaamini shida ni apu, tuma ujumbe kwa mtunzi na maelezo yanayofuata. Ujumbe bila maelezo hayataangaliwa, maanisha yatapuuzwa.

- Aina ya kifaa
- Maelezo ya msingi ya nini haifanyi kazi: kuacha kufanya kazi? haiwezi chungua? inaonekana ajabu?
- Je, unakubali kwamba ulijaribu hatua zilizo hapo juu kwanza
- Rekodi ya kumbukumbu ya kifaa ilipoanza
