Apu maalum ya Android ya Wikipedia iliyobuniwa kusaidia kupata, kufichua na kupeleleza maarifa iliyo Wikipedia. Suluhisha dau na rafiki yako kwa kutafuta haraka kwenye apu, ama zamia kwenye makala yaliyoangaziwa, picha, nakala iliyopendekezwa na mengine mengi kwa kutumia bibu ya upelelezi. Kwa zaidi ya makala milioni 39 katika takriban lugha 300, ensaiklopidia yako ya mtandaoni unayoipenda zaidi iko mikononi mwako.

Vipengele:

Uwezo wa kutafuta kwa sauti - Pata kwa urahisi unachokitafuta kwa upau maarufu wa utafutaji juu ya apu, ikiwa pamoja na utafutaji unaowezeshwa kwa kutamka kwenye kifaa chako.

Tuma maoni yako kuhusu apu! Kwa menu,bonyeza "Settings", kisha" About the wikipedia app",kisha "Send app feedback".

Sera ya faragha: https://m.wikimediafoundation.org/wiki/Privacy_policy

Masharti za kutumika: https://m.wikimediafoundation.org/wiki/Terms_of_Use

Kuhusu Msingi wa Wikimedia

Msingi wa Wikimedia ni shirika lisilo la faida linalo fadhili Wikipedia na miradi mingine ya Wikimedia. Msingi huu ni wa hisani na hufadhiliwa hasa kwa michango. Kwa maelezo zaidi, zuru tovuti yetu:https://wikimediafoundation.org/wiki/Home.
