DictionaryForMIDs ni kamusi inayoweza kuanzishwa na lugha zote ulinmwenguni. Kwa mfano inawezekana kusanidi DictionaryForMIDs na kamusi ya Kiingereza hadi Kihispania na pia kwa kamusi ya Kiingereza hadi Kichina.

Zaidi ya kamusi za lugha, inawezekana kusanidi kamusi nyingine yoyote ya DictionaryForMIDs, kwa mfano kamusi ya ZIP, kamusi ya simu, kamusi ya maneno ya matibabu, n.k.

Tafadhali kumbuka kuwa kamusi ambazo zimeundwa kwa DictionaryForMIDs zinaweza kuwa na hakimiliki tofauti. Kamusi zote zinazoweza kupakuliwa kutoka kwa tovuti ni bure kutumia. Kamusi ainati zimekuja na apu na zaidi hutolewa katika sehemu ya kamusi za kupakua kwenye tovuti.
