OsmAnd+ (OSM Automated Navigation Directions) ni ramani na apu ya uongozaji safari iliyo na uafikiaji wa data ya bure, ulimwenguni kote, na ya ubora wa juu ya OpenStreetMap (OSM). Furahia kuongozwa kwa sauti na macho, kutazama POI (mambo ya kuvutia), kuunda na kudhibiti mikokoto za GPX, kutumia taswira ya mistari ya kontua na maelezo ya mwinuko, chagua kati ya kuendesha gari, kuendesha baiskeli, njia za watembea kwa miguu, uhariri wa OSM na mengine mengi.

OsmAnd+ ni toleo kamili ya apu hii. Tafadhali changia ili kusaidia mradi huu, kufadhili kutengenzwa kwa vipengele vipya, na upokee masasisho ya hivi punde.

Baadhi ya vipengele vikuu:
Urambazaji
 • Inafanya kazi mtandaoni (haraka) au nje ya mtandao (hakuna gharama za kutumia mitandao ya ng'ambo ukiwa nje ya nchi)
 • Uelekezi wa sauti (sauti zilizorekodiwa na kusanisi)
 • Uelekezi wa hiari wa njia, onyesho la jina la mtaa, na makadirio ya muda wa kuwasili
 • Inaauni pointi za kati kwenye ratiba yako
 • Uelekezaji upya kiotomatiki kila unapotoka kwenye njia
 • Tafuta maeneo kwa anwani, kwa aina (k.m.: mkahawa, hoteli, kituo cha mafuta, makumbusho), au kwa kuratibu za kijiografia

Kuangalia Ramani
 • Onyesha msimamo na mwelekeo wako
 • Pangilia picha kwa hiari kulingana na dira au mwelekeo wako wa mwendo
 • Hifadhi maeneo yako muhimu zaidi kama Vipendwa
 • Onyesha POI (sehemu za kupendelewa) karibu nawe
 • Onyesha vigae maalum vya mtandaoni, mwonekano wa setilaiti (kutoka Bing), viwekeleo tofauti kama vile kutembelea/kuvinjari njia za GPX na safu za ziada zenye uwazi unaoweza kugeuzwa kukufaa
 • Kwa hiari onyesha majina ya sehemu mbalimbali kwa tahajia ya Kiingereza, ya ndani au ya kifonetiki

Tumia data ya OSM na ya Wikipedia
 • Maelezo ya ubora wa hali ya juu kutoka kwa miradi bora zaidi ya ushirikiano duniani
 • Data ya kila nchi au eneo inapatikana kwa OSM
 • Wikipedia POIs, nzuri kwa kutalii
 • Vipakuliwa bila kikomo , moja kwa moja kutoka kwenye apu
 • Ramani za vekta za nje ya mtandao zinazosasishwa angalau mara moja kwa mwezi
 
 • Uteuzi kati ya data kamili ya eneo na mtandao wa barabara pekee (Mfano: Japani yote ni MB 700 au MB 200 kwa mtandao wa barabara pekee)

Vipengele vya usalama
 • Kubadilisha mwonekano wa mchana/usiku otomatiki kwa hiari 
 • Onyesho la hiari la kikomo cha kasi, pamoja na kikumbusho ukizidisha
 • Kukuza kwa hiari kutegemea kasi
 • Ambia marafiki zako eneo lako ili wakupate

Vipengele vya Baiskeli na Watembea Miguu
 • Kuangalia njia za miguu, kupanda kwa miguu na baiskeli, nzuri kwa shughuli za nje
 • Njia maalum za kuelekeza na kuonyesha kwa baiskeli na watembea miguu
 • Vituo vya hiari vya usafiri wa umma (basi, tramu, treni) ikijumuisha majina ya laini
 • Hiari ya kurekodi safari kwa faili ya GPX au huduma ya mtandaoni
 • Onyesho la hiari la kasi na mwinuko
 • Onyesho la mistari ya kontua na utiaji kivuli (kupitia programu-jalizi ya ziada)

Changia Moja kwa Moja kwa OSM
 • Ripoti hitilafu za data
 • Pakia njia za GPX kwenye OSM moja kwa moja kutoka kwa apu
 • Ongeza POI na uzipakie moja kwa moja kwenye OSM (au baadaye ikiwa nje ya mtandao)
 • Uwezo wa kurekodi safari kwa hiari katika hali ya chinichini (kifaa kikiwa katika hali tuli)
OsmAnd ni programu huria na inaendelezwa kikamilifu. Kila mtu anaweza kuchangia kwenye apu hii kwa kuripoti hitilafu, kuboresha tafsiri au kuunda vipengele vipya. Mradi uko katika hali changamfu ya uboreshaji unaoendelea na aina hizi zote za mwingiliano wa developa wa apu na watumiaji. Maendeleo ya mradi pia unategemea michango ya kifedha kufadhili uwekaji misimbo na majaribio ya utendaji mpya.
Makadirio ya utandawazi wa ramani na ubora:
 • Ulaya Magharibi: ****
 • Ulaya Mashariki: ***
 • Urusi: ***
 • Amerika Kaskazini: ***
 • Amerika Kusini: **
 • Asia: **
 • Japani & Korea: ***
 • Mashariki ya Kati: **
 • Afrika: **
 • Antaktika: *
Nchi nyingi duniani zinapatikana kama vipakuliwa!
Kutoka Afghanistan hadi Zimbabwe, kutoka Australia hadi Marekani. Argentina, Brazili, Kanada, Ufaransa, Ujerumani, Mexico, Uingereza, Uhispania,…

Mapambano ya Vipengele:
* Rasilimali isiyo bure- Kazi ya sanaa na mipangilio yako chini ya leseni isiyo ya kibiashara.
