Kumbuka: F-Droid inahitaji upendeleo wa mizizi ili kusimika Kiendelezi cha Upendeleo kama mfumo wa "priv-app".

https://f-droid.org/packages/org.fdroid.fdroid inaweza kutumia haki za mfumo au ruhusa kusimika, kusasisha na kuondoa apu kivyake. Njia pekee ya kupata mapendeleo hayo ni kuwa apu ya mfumo.

Hapa ndipo Ugani wa Upendeleo unapoingilia- kwa sababu ni apu tofauti ambayo ni ndogo zaidi, inawezasimikwa kama apu ya mfumo na iwasiliane na apu kuu kupitia AIDL IPC.

Hii iko na faida kadhaa:

* Matumizi pungufu ya diski katika kitenganishi cha mfumo
* Masasisho ya mfumo hayaondoi F-Droid
* Mchakato wa kusimika kwenye mfumo kupitia mzizi ndio salama zaidi

Hii imefungwa kama faili ya sasisho la ZIP kwa mbinu ya OTA (Over-The-Air). Ni lazima isakinishwe kutumia TWRP au urejeshaji mwingine wa Android ambao unawezaonyesha masasisho kwenye mfumo kutoka folda ya /data/data/org.fdroid.fdroid iliyo katika kitenganishi cha /data. Hii APK inayosimama pekee yake inaitwa katika https://f-droid.org/packages/org.fdroid.fdroid.privileged, na hiyo inatoa masasisho baada ya hii kifurushi cha OTA kusimikwa.
